Hivi Sir Alex Ferguson anataka kumaliza kipaji cha Rooney??? Imepita mwaka sasa tokea Rooney abadilishwe nafasi kutoka ushambuliaji hadi kuwa kiungo. Tokea Rooney aanze kucheza nafasi ya kiungo amekuwa akichemsha sana lakini Sir Alex hajataka kulifanyia kazi zaidi ya kuendelea kumpanga kama kiungo. Picha hii inamuonesha Rooney akitoka dakika ya 71 katika mechi kati ya West Ham na Man utd ambapo Rooney alikuwa akicheza nafasi ya kiungo, lakini alishindwa kabisa kuimudu jambo lililofanya atolewe na kuingia Giggs. |
No comments:
Post a Comment