|
David James |
David James golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya England amesema
makocha wenye asili ya Kiafrika hawapati nafasi ya kufundisha klabu kubwa kwenye
ligi ya England kwasababu hawana uwezo wa kutosha. Akiongea na gazeti la Sport
360 James alisema “makocha weusi hawana uwezo, hakuna haja ya kuwapa kazi ya ukocha,
wamiliki wengi wa timu za mpira wapo tayari kusajili wachezaji weusi ila sio makocha weusi
kwasababu hawana vigezo vya kufundisha timu kubwa".
|
Chri Hughton |
James aliendelea kusema, "kati ya klabu 92 za England
kuna makocha weusi watano tu na kati ya hao ni kocha mmoja tu aliyefanikiwa
ambaye ni kocha wa Norwich Chri Hughton. Hughton amefanikiwa kwasababu ana
utaratibu mzuri wa yale anayoyapanga na kuyafanya, lakini wengine wote waliobakia
hawawezi kufika popote na sio kweli kwamba jambo hili linahusisha ubaguzi wa
rangi kama vile wengi wanavyofikiria” hayo ni maneno ya James ambaye alishawahi
kuwa mchezaji wa Liverpool, Man City na Aston Villa kwasasa yupo nchini Iceland
kwenye klabu ya IBV.
No comments:
Post a Comment