Tuesday, April 2, 2013

Big mechi leo PSG na Barcelona


PSG na Barcelona wanakutana leo katika mechi ya robo fainali katika mashindano ya UEFA. PSG wakiwa nyumbani watahitaji ushindi ili wajiweke kwenye mazingira mazuri ya kusonga mbele. Kocha wa PSG Carlos Ancelotti amesema kwenye mechi ya leo hawatacheza mchezo wa kuzuia kama timu zingine zinavyochezaga zikikutana na Barcelona, "sisi tutashambulia mwanzo mwisho" alisema Ancelotti. Kikosi cha PSG leo kitakuwa “full” baada ya UEFA kumruhusu Ibrahimovic kucheza kwenye mechi ya leo kufuatia kadi mbili za njano alizopewa kwenye mechi ya kwanza na Valencia. 

PSG wakiwa kwenye mazoezi
PSG watakuwa wakimtegemea zaidi Ibra na Pastore katika ushambuliaji dhidi ya ngome dhaifu ya Barcelona wakati wao Barcelona watamtegemea zaidi Iniesta na Messi kwenye safu ya ushambuliaji wakisaidiana na Alexis au Villa ambao watacheza badala ya Pedro ambaye ni mgonjwa. 

Mashabiki wengi duniani wanangojea kwa hamu mchezo wa leo ili kupima uwezo wa PSG timu ambayo inakuja kwa kasi katika soka, vilevile kuona mchezo mzuri kati ya miamba hiyo miwili yenye wachezaji wazuri wenye vipaji na pia kumuona Beckham ambaye amerudi Ulaya akitokea Amerika. 
Kocha wa Barcelona Tito (wa nyuma) akishuka kwenye ndege jijini Paris, hii itakuwa mechi yake ya kwanza baada ya kurudi kutoka kwenye matibabu ya kansa
Beckham akiwa mazoezini leo asubuhi,mechi ya leo itakuwa muhimu kwake kuonesha uwezo wake

Matarajio ya vikosi vya leo ni

PSG: Sirigu; Wiel, Alex, Silva, Maxwell; Moura, Verratti, Matuidi, Pastore; Ibrahimovic, Lavezzi. 

Barcelona: Valdes, Alves, Mascherano, Pique, Alba, Busquets, Xavi, Iniesta, Cesc, Messi, Villa

No comments:

Post a Comment