Uongozi wa Simba umesema utafanya mkutano mkuu July mwaka
huu. Maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao kilichoongozwa na mwenyekiti wake
Aden Rage. Katika taarifa zake, uongozi wa Simba umesema tarehe halisi ya kufanya
mkutano huo itatangazwa muda ukikaribia. Uongozi wa Simba umefikia hatua hii
baada ya baadhi ya wanachama wake kufanya mkutano mwezi uliopita, mkutano ambao ulisemekana kuwa ni
batili na kuchagua viongozi wapya. Katika mkutano mwezi July, wanachama wa Simba watakutana ili kuzungumzia maswala muhimu ya club
hiyo ikiwemo matokeo mabovu ya club hiyo kwenye ligi kuu Tanzania bara.
No comments:
Post a Comment