Leo usiku kutakuwa na mechi ya robo fainali kati ya Real
Madrid na Galatasaray mchezo utakaofanyika saa tatu na dakika 45 usiku kwa saa
za Afrika mashariki. Mechi hii kwa leo ndiyo inasubiriwa kwa hamu na wapenzi
wengi wa mpira tofauti na mechi kati ya Malaga na Borussia Dortmund ambayo
haina msisimko mkubwa. Katika mechi ya leo kati ya Real na Gala, Madrid
wanatarajiwa kushinda ili waweze kujiwekea matumaini ya kusonga mbele kwani
watakuwa wakicheza kwenye uwanja wa nyumbani. Wikiendi iliyopita Madrid waliwapumzisha
nyota wake wote kwa ajili ya mechi ya leo.
Naye kocha wa Madrid, Mourinho amesema leo watacheza
kuhakikisha wanashinda ili mchezo wao wa marudiano uwe mwepesi. Aliongeza kwa
kusema Drogba na Sneijder nawajua ni wachezaji wazuri sana lazima tuhakikishe
hawapati nafasi za kucheza na mpira.
Katika mechi ya leo kinachosubiriwa kwa hamu ni kuona kama
kikosi cha Mourinho kitaweza kuwazuia Drogba na Sneijder wachezaji ambao Mourinho amesema anawajua nje ndani.
Pia Ronaldo atakuwa kwenye harakati ya kuhakikisha anafunga ili aweze kumpita mpinzani wake Messi wakiwa wote wana magoli 8 hadi sasa. Vilevile, Madrid na Gala wote wanacheza mchezo
unaofanana na wanawachezaji wenye uwezo mkubwa hivyo wapenzi wa soka
wanategemea kuona mchezo mzuri wenye ushandani. USIKOSE leo usiku saa tatu dk 45.
No comments:
Post a Comment