Kampuni ya Beinjing Cosntruction Engineering Group (BCEG) kutoka nchini China, ambayo mwishoni mwa mwaka jana ilisaini makubaliano ya upembuzi yakinifu juu ya ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu (Kaunda stadium) leo imewasilisha michoro na makadirio ya bajeti ya ujenzi wa Uwanja mpya eneo la Jangwani. Kaunda stadium utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 40,000, waliokaa kwenye viti, huku ukiwa na sehemu za maegesho ya magari, sehemu ya watu maarufu (VIP) hostipali, hoteli na hosteli, eneo la waandishi wa habari, eneo la walemavu na huduma zote muhimu zinazopatikana katika viwanja vya michezo. Kwa mujibu wa makubaliano ya kampuni ya BCEG na klabu ya Yanga ujenzi wa uwanja mpya wa Kaunda stadium utachukua muda wa miaka miwili, kuanzia utakapoanza ujenzi wake ambapo unatazamiwa kuanza mwezi wa Julai 2013 kulingana na kukamilika kwa taratibu za ujenzi kwa kampuni hiyo.Hongera Yanga kwa kufikia hatua hii.
|
Uwanja wa Yanga kwa ndani utakavyokuwa |
|
Uwanja utakavyokuwa kwa nje |
No comments:
Post a Comment