Msemaji wa Yanga bwana Baraka Kizuguto amesema klabu ya Yanga inahitaji kupigiwa makofi ya heshima kama mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara
mwaka huu. Klabu ya Yanga ambayo imeshatangazwa mabingwa ikiwa wamebakiza mechi
mbili, wamehitaji siku ya mechi yao inayofuata dhidi ya Coastal Union wachezaji
wa Coastal wapange mistari miwili huku wachezaji wa Yanga wakipita katikati kwa
kupigiwa makofi kama wananyofanya kwenye ligi za Ulaya. Kitendo hiki cha
kupigiwa makofi ya heshima ni kawaida kufanyika katika ligi za ulaya mfano Man
utd walipigiwa makofi na timu ya Arsenal katika mechi ya jumapili iliyopita
kama mabingwa wa ligi ya Uingereza mwaka huu. Lakini alipoulizwa katibu mkuu wa
TFF bwana Angetile Osiah kuhusiana na jambo hilo alisema Yanga
haitaweza kufanyia kitendo hicho kwasababu katiba ya sasa ya TFF hairuhusu
kufanya kitendo hicho kwahivyo itakuwa ni vigumu kwa Yanga kupewa heshima hiyo
na Coastal Union, ila bwana Osiah amesema jambo hilo ni zuri litazingatiwa ili
liwepo kwenye katiba ya TFF. Kitendo hiki cha kupiga makofi ya heshima
kimeanzia barani Ulaya ikiwa ni moja ya jitihada ya vyama vya soka duniani
kuhamasisha “fair play” hivyo TFF ni vyema wakalifanyia kazi jambo hili kwani
mashabiki wa soka Tanzania wanangojea kwa hamu kuona Simba au Yanga inampigia
makofi mwenzake, licha yakuwa tukio hilo litakuwa la kihistoria kwenye soka la
bongo.
Tukio hili la kupigiwa makofi ya heshima lilitokea jumapili iliyopita Arsenal walipowapigia makofi Man utd kama mabingwa wa kombe la ligi kuu nchini Uingereza, kitendo kama hiki ndicho Yanga wamehitaji kufanyiwa katika mechi yao inayokuja dhidi ya Coastal Union. |
No comments:
Post a Comment