Kiungo wa Man City Yaya Toure leo amesaini mkataba mpya na
club yake baada ya vuta nikuvute ya wiki mbili. Yaya Toure aliomba mkataba mpya mwishoni mwa mwezi uliopita lakini club yake ilikuwa na kigugumizi
hadi kupelekea kutoelewana kati ya Seluk wakala wa Toure na uongozi wa Man
City. Hatua hiyo ili sababisha wakala huyo kukasirika na kutamka hadharani kuwa Toure yupo
tayari kuhama City kama mkataba mpya utashindikana. Kufuatia hali hiyo, Club nyingi zikiwemo
Chelsea na Madrid walionesha nia ya kumnunua Yaya lakini leo imekuwa mwisho wa
yote baada ya Toure kukubaliana na City kwa kusaini mkataba wa miaka minne wenye
thamani ya paundi milioni 11.
No comments:
Post a Comment