Ashley Cole amenyakwa na kamera za mapaparazi akivuta sigara wikiendi hii mjini Los Angeles nchini Marekani. Cole amefaya kitendo hiki huku akijua ni kinyume na sheria za klabu yake licha ya kuwa amekifanya akiwa likizo. Baadhi ya marafiki zake wamesema mara kadhaa mchezaji huyo huwa anavuta sigara bila kujali afya yake ikilinganishwa na aina ya kazi yake inayohitaji mtu mwenye mapafu salama na yenye afya. Rafiki zake wamesema mbali ya kumuonya mara kwa mara lakini Cole bado anaendelea kupiga fegi kama kawaida. Msimu uliopita Jose Mourinho alipokuwa akiifundisha Madrid alimpiga benchi kwa muda mrefu beki wa klabu hiyo Fabio Coentrao baada ya kudakwa na mashushu wa klabu akivuta sigara hivyo Cole anaweza pia kupatwa na balaa kama la Coentrao asipokuwa makini. |
Sunday, June 16, 2013
Ashley Cole adakwa na kamera akipiga fegi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment