Baada ya kutangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Chelsea, Jose Mourinho ameshawataja wachezaji anaowahitaji ndani ya klabu ili timu aweze kufikia malengo aliyopewa na Bosi Chelsea Roman Abramovich. Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Chelsea, zilizoelezwa na gazeti la Sportmail zinasema, Mourinho anawahitaji wachezaji watano ambao ni Dzeko (Mshambuliaji-Man city), Mangala (Beki wa kati-Porto), De Rossi (Kiungo-Roma), Fernandinho (Kiungo-Donetsk) na Jovetic (Mshambuliaji-Fiorentina). Mahitaji haya ya Mourinho yanaonesha wazi kuwa klabu ya Chelsea ina mapungufu kwenye idara zote kuanzia ulinzi, katikati na ushambuliaji ndiyo maana Mourinho amewahitaji wachezaji hao wote. Taarifa hizi zinadhibitisha tetesi zilizokuwepo kuwa kuna baadhi ya wachezaji Mourinho hataki kuwaona Chelsea akiwemo David Luiz, hivyo baada ya usajili kukamilika ataiomba klabu iwauze wote ambao anaona hawana manufaa. Chelsea inatarajia kuanza kufanya usajili wiki hii ili kutimiza mahitaji ya Mourinho kabla maandalizi ya msimu ujao hajaanza. |
Tuesday, June 4, 2013
Mourinho atangaza kuwasajili wachezaji wa tano
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment