Mkongwe Roberto Carlos amemshauri mchezaji mwenzake wa
zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane akubali kuwa kocha wa Madrid kwasababu uwezo
wa kuifundisha timu hiyo anao. Carlos aliongea hayo kupitia gazeti la Marca la
nchini Hispania akisema ‘namshauri Zidane akubali kuifundisha Real Madrid, asijifikirie kuhusu uwezo wake kwani Zidane ana uwezo kuifundisha Madrid, ana uwezo wa
kusoma mchezo, ana uwezo pia wa kuwaunganisha wachezaji na kila jambo analolifanya huwa ana uhakika nalo habahatishi, atashinda
vikombe vingi sana, ninaongea hivi kwasababu
nilikuwa naye Madrid hivyo nina mjua vizuri sana Zidane’. Maneno haya ya Carlos
yamekuja baada ya tetesi kuvuma kuwa Zidane bado anajifikiria kuhusu ofa aliyopewa ya kuifundisha
Madrid baada ya PSG kugoma kumwachia Ancelotti kuhamia Madrid. Kwasasa
Zidane ni mshauri wa masuala ya usajili wa Madrid na kazi aliyopewa msimu huu
ni kuhakikisha Gareth Bale wa Tottenham anatua Madrid.
No comments:
Post a Comment