Bingwa wa dunia wa tenesi kwa upande wa wanawake Serena Williams leo ameaga mashindano ya Wimbledon baada ya kupigwa na Mjerumani Sabine Lisicki kwa seti 6-2, 1-6 na 6-4. Matokeo ya leo yamemalizia maajabu yaliyotokea kwenye michuano hii mwaka huu baada ya mabingwa wengine wakubwa kutolewa kwenye hatua za mwanzo, jambo ambalo limeifanya michuano hii kukosa hamasa, mastaa wengine waliotoka ni Sharapova, Azarenka, Caroline Wozniacki n.k. Matokeo haya yanamfanya Lisicki aingie kwenye robo fainali na atakutana na Kaia Kanepi. |
No comments:
Post a Comment