Howard Webb ndiye refa aliyechaguliwa na FA kuchezesha mechi kati ya Man city na Man utd, mechi ambayo ni ya upinzani wa timu za jiji la Manchester. Kuchaguliwa kwa Webb kuchezesha mechi hii kumeleta mzozo kwa washabiki wa Man city kutokana tetesi zilizopo kuwa Webb ni kipenzi cha Man utd. Mara kadhaa refa huyu akichezesha mechi kati ya Man utd na timu nyingine, washabiki wa timu pinzani na Man utd wamekuwa wakimlalamikia kuipendelea Man utd. Lakini Webb mwenyewe amesema hayo ni maneno ya washabiki, yeye hana mapenzi yoyote na Man utd. Mbali ya kutajwa na baadhi ya watu kuipendelea Man utd, Webb bado amebakia kuwa refa tegemezi wa FA ambaye anaaminika kuchezesha mechi kubwa za ligi ya Uingereza na pia amekuwa akichaguliwa mara kadhaa na FIFA kuchezesha mechi kubwa za dunia. |
Monday, September 16, 2013
Howard Webb kuchezesha Manchester derby
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment