Klabu ya Real Madrid na uongozi wake umeanza kutambua mchango wa Ozil mchezaji aliyeuzwa kwenda Arsenal katika dakika za mwisho mwisho. Uamuzi wa kumuuza Ozil ulikuja baada ya Madrid kumsajili Bale na kuridhishwa na kiwango cha Isco mchezaji aliyesajiliwa kutoka Malaga. Lakini wikiendi hii Real Madrid walitambua mchango wa Ozil baada ya kufungwa na Atletico Madrid kwenye uwanja wa nyumbani. Katika mchezo huo klabu ya Real Madrid ilishindwa kabisa kupenya kwenye ngome ya At. Madrid jambo ambalo lilikuwa ni rahisi kwa Ozil. Kocha Ancelotti atakuwa kwenye wakati mgumu kuijenga upya Madrid ili iweze kucheza na kushinda kama ambavyo washabiki wake wanatarajia. Hali inakuja baada ya washabiki wengi wa Madrid kukerwa na kitendo cha Ozil na Kaka kuuzwa.
Ozil tokea ahamie Arsenal ameonesha kiwango kizuri na ameweza kurudisha imani kwa washabiki wa Arsenal ambao kwa miaka kadhaa walikuwa hawana imani na timu yao kupigania ubingwa. Lakini ujio wa Ozil umeleta hamasa kubwa ndani ya klabu, jambo ambalo linawauma washabiki na viongozi wa Real Madrid, kwani hadi sasa Ozil ameshaweza kutoa pasi za mwisho tatu zilizozaa magoli na klabu ya Arsenal inaoongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 15.
|
Monday, September 30, 2013
Pengo la Ozil limeanza kuonekana Real Madrid
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment