Wachezaji wa klabu ya Barcelona wakiteremka kwenye ndege ya shirika la Iberia nchini Scotland tayari kuwakabili wababe wao Celtic kwenye michuano ya Uefa Champions. Katika mchezo wa leo Barcelona watamkosa mshambuliji wao tegemezi Lionel Messi ambaye ni majeruhi baada ya kuumia paja wikiendi iliyopita. Mbali ya Messi, Barcelona itawakosa pia Jordi Alba, Javier Mascherano, Carles Puyol, Isaac Cuenca na Ibrahim Afellay ambao wote ni majeruhi. Msimu uliopita Barcelona walifungwa goli 2-1 na Celtic nchini Scotland, jambo ambalo linaufanya mchezo wa leo kuwa wa kuvutia, kwani Barcelona watataka kurudisha heshima yao wakati Celtic watataka kuendeleza ubabe. |
No comments:
Post a Comment