Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho jana alikatiza mkutano na waaandishi habari baada ya kukerwa na maswali kumhusu Kevin de Bruyne. Mourinho aliingia kwenye ukumbi wa maelezo kuongea na waandishi wa habari kwa kujiamini na alianza kumuongelea Mata akisema ‘Mata safari hii atacheza kwenye mechi dhidi ya Steaua’, Mourinho aliongea hivyo akifahamu fika waandishi watamuuliza kuhusu Mata. Lakini mambo yakawa tofauti, na waandishi safari hii walimuuliza kuhusu De Bruyne, mchezaji ambaye hakuwepo kwenye orodha ya kucheza, na ndipo hapo Mourinho alipochukia akisema ‘kwa majuma matatu mmekua mkiongea kuhusu Mata, na sasa zamu ya De Bruyne, kwa hiyo nyinyi mnashughulishwa sana na wachezaji wasiocheza badala ya wanaocheza?" Baada ya kuhoji hayo Mourinho alisimama na kuondoka ndani ya chumba cha mkutano, waandishi wakabaki wanaangaliana tu. Unaweza kuangalia tukio hili kwenye video hapo chini.
Mourinho akitoka nje ya ukumbi baada ya kuchukizwa na waandishi wa habari |
No comments:
Post a Comment