Kiungo mpya wa Arsenal, Mesut Ozil ameendelea kung'arisha nyota yake akiwa na klabu ya Arsenal. Katika mechi ya jana usiku Uefa Champions dhidi ya Napoli, Ozil alicheza mpira safi uliovutia jambo ambalo limemfanya kocha wa Arsenal, Arsene Wenger kujisikia furaha kwa kuona mchezaji aliyemnunua kwa bei kubwa analeta faida zaidi ya pesa iliyotumika. Mbali ya kucheza vyema katika mechi ya jana, Ozil pia alifanikiwa kufunga goli zuri, goli ambalo linatarajiwa kuwa moja kati ya magoli bora kwenye michuano ya Uefa msimu huu. Kuthibitisha hili, magezeti karibia yote ya michezo nchini Uingereza na kwenye baadhi ya nchini yamepambwa na kicha za habari kikuu kuhusu Ozil na goli alilofunga. Chini ni baadhi ya picha na video kuhusu Mesut Ozil.
|
Magazeti ya Uingereza yalivyopendeza na jina la Ozil leo asubuhi |
|
Ozil akiangalia mpira alioupiga ukielekea nyavuni |
|
Ramani ya jinsi goli lilivyofungwa na Ozil |
Video inayoonesha goli lilivyofungwa
No comments:
Post a Comment