Picha ni timu ya Chelsea ikiwa mazoezini kujiandaa na mechi ya leo dhidi ya Steaua Bucharest katika mchezo wa kundi E Uefa Champions. Chelsea wanaingia dimbani leo usiku wakiwa na rekodi ya kufungwa nyumbani na klabu ya FC Basel, hivyo mchezo wa leo ni lazima washinde ili wajiweke katika mazingira mazuri ya kusonga mbele. Katika mahojiano na waandishi wa habari kocha Jose Mourinho na kiungo Frank Lampard wamekiri kuwa leo usiku watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Steaua, kwani watakuwa ugenini kucheza na timu ambayo imedhamiria kushinda mchezo wake wa kwanza wa nyumbani. Lakini wametoa ahadi kwa wapenzi wao kuwa watapigana kufa na kupona ili washinde mchezo wa leo. Mourinho katika maelezo yake alisisitiza kuwa wanatarajia kukutana na mchezo mgumu lakini kushinda ni jambo la lazima kwa Chelsea.
No comments:
Post a Comment