Vita kati ya Higuain na Arsenal
Mechi ya leo kati ya Arsenal na Napoli inamkutanishia Gonzalo Higuain pamoja na Arsenal, klabu ambayo Higuain alikataa kujiunga nayo na kuichagua Napoli. Katika mchezo huu Higuain atataka kuonesha kuwa klabu aliyoichagua ni bora kuliko Arsenal, lakini Arsenal pia watataka kumuonesha wao ni wababe zaidi. Mbali na hilo, mashabiki wa Arsenal wameshajipanga kumzomea Higuain kwa kitendo cha kuikacha klabu yao ambayo hadi sasa inahangaika kutafuta mshambuliaji wa mwisho.
Gonzalo Higuain |
Vita kati ya Arsene Wenger na Rafa Benitez
Arsene Wenger na Rafa Benitez ni maadui katika soka kwa muda mrefu kwani kabla ya Benitez kujiunga na Napoli alikuwa ni kocha wa Liverpool na Chelsea. Wenger atamkumbuka zaidi Benitez baada ya Liverpool kuitoa Arsenal kwenye robo fainali ya Uefa champions mwaka 2008. Machungu ya kutolewa na Liverpool iliyokuwa chini ya Benitez bado yapo kwenye fikra za Wenger ili kulipiza kisasi. Alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Wenger alisema 'natambua Benitez ni kocha mzuri, na uwezo wake mkubwa ni kuijenga timu inayofanya mashambulizi ya kushitukiza na kukaba mpira kwa nguvu zote, hivyo na sisi tumejipanga kubalina na haya yote'.
Arsene Wenger na Rafa Benitez
Ozil vs Higuain, Albiol na Callejon
Katika mechi ya leo Ozil atakuwa akicheza dhidi ya wachezaji wenzake wa zamani aliokuwa nao Madrid ambao ni Higuain, Albiol na Callejon. Kupitia akaunti yake ya twitter Ozil alisema anangojea kukutana tena na Higuain, Albiol na Callejon lakini watamsamehe kwasababu hana chochote cha kuwapa.
Kinyang'anyiro cha kuongoza kundi F
Utamu mwingine wa mechi kati ya Arsenal na Napoli ni kwamba timu zote mbili zinaoongoza kundi kwa idadi sawa ya kila kitu (pointi na magoli), hivyo leo kila timu itapigana ili kushika nafasi ya kwanza. Kama inavyoonekana hapo chini ni msimamo wa kundi F.
Group F
Clubs | P | W | D | L | F | A | +/- | Pts |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Arsenal FC | 1 | 1 | 0 | 0 | 2 | 1 | 1 | 3 |
SSC Napoli | 1 | 1 | 0 | 0 | 2 | 1 | 1 | 3 |
Dortmund | 1 | 0 | 0 | 1 | 1 | 2 | -1 | 0 |
Marseille | 1 | 0 | 0 | 1 | 1 | 2 | -1 | 0 |
Mazoezi ya mwisho mwisho ya timu zote mbili Arsenal na Napoli
No comments:
Post a Comment