Wilfried Zaha ni mchezaji mpya wa Man utd aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace, timu ambayo imepanda daraja kucheza ligi kuu nchini England msimu huu na Zaha ndiye mchezaji aliyeiwezesha timu hiyo kwa kiasi kikubwa hadi kupanda daraja. Baada ya kuhamia Man utd, Zaha alifanikiwa kupata nafasi ya kutosha kuonesha uwezo wake kwenye mechi za kirafiki za Man utd barani Asia. Lakini tokea ligi ianze Zaha hajaweza kupata nafasi ya kucheza kwenye mechi hata moja na tetesi zilizopo ni kuwa, Moyes ameamua kumpiga chini Zaha kwasababu alitembea na binti yake. Taarifa hizi za Zaha kukutwa faragha na binti wa Moyes zimeanza kuzagaa wiki hii baada ya watu kuhoji kwanini Zaha hapati nafasi. Wawili hawa inasemekana walifanya mahusiano yao kwa siri kubwa ili kuepusha mahusiano mabaya kati ya Zaha na Moyes, lakini kwa bahati mbaya habari ndiyo zimeshamwagika. Zaha mwenyewe kupitia akaunti yake ya twitter amekanusha taarifa hizi akisema ni uongo, ila haijajulikana hadi sasa uongo ni upi kati ya yeye kutoka na mtoto wa Moyes au kutopangwa kwasababu anatoka na mtoto wa Moyes. Lakini, ukweli utabaki palepale kuwa, Zaha hawezi kusema ukweli kwasababu Moyes ni bosi wake ndiyo maana majibu ya Zaha watu wameyatupilia mbali. Chini ni majibu ya Zaha kupitia akaunti yake ya twitter na pichani hapo juu ni binti wa Moyes |
Tuesday, October 1, 2013
Tuhuma za Zaha kutoka na mtoto wa Moyes
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment