Baada ya kufunga magoli matatu dhidi ya Man utd, mshambuliaji wa Chelsea Samwel Eto'o anatarajiwa kuondoka darajani mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na klabu yake iliyomtoa Real Mallorca. Eto'o aliyasema hayo jana wakati akiongea na radio ya Hispania COPE. Eto'o alisema ndoto zake ni kumalizia soka kwenye klabu ya Mallorca na mkataba wake na Chelsea unakwisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo baada ya mkataba kuisha atajiunga na Mallorca kama mchezaji huru.
Gazeti la Italia, Corriere Dello Sport,linaripoti kuwa beki wa Arsenal, Thomas Vermaelen anawindwa na klabu ya Napoli ya nchini humo kwa ofa ya Euro 5.5 mil. Dello limesema Vermaelen mwenyewe yupo tayari kujiunga na Benitez ili aweze kucheza mechi nyingi kabla ya kombe la dunia ambapo atajiunga na timu yake ya taifa Belgiam. Ushindani wa namba anaoupata Vermaelen dhidi ya Laurent Koscielny na Per Mertesacker ndiyo unamfanya akae benchi kwa muda mrefu jambo ambalo linampotezea nafasi pia kwenye kikosi cha timu ya taifa.
Klabu tajiri duniani Real Madrid imeripotiwa kuwa ipo kwenye mipango ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Bayern Munich, Thomas Müller. Taarifa hizi zimetolewa na gazeti la Hispania Marca na usajili huu unatarajiwa kufanywa mwishoni mwa msimu kabla ya kombe dunia kuanza.
Mkurugenzi wa benchi la ufundi wa klabu ya Atletico Madrid, Andrea Berta amesema klabu yake itatumia gharama zozote kuwabakiza mastaa wake akiwemo Diego Costa. Berta ameongea haya mbele ya waandishi wa habari kutokana uvumi uliopo kuwa Costa na Koke wanaweza kuhama Atl. Madrid ndani ya dirisha dogo kwenda EPL. Klabu za EPL ambazo zimetajwa kuwahitaji wachezaji hawa ni pamoja na Chelsea, Man utd na Arsenal. Klabu ya Atl. Madrid ni moja ya klabu ambazo zinatengeneza wachezaji wazuri na kuwauza kwenye klabu kubwa, lakini safari hii klabu hii imegoma kuwauza wachezaji wake baada ya kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya Uefa champions.
Mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao amevunja ukimya baada ya kutangaza waziwazi kuwa yeye hana mpango wa kwenda Chelsea. Falcao amesema hayo baada ya kuulizwa kuhusu tetesi za kuhamia Chelsea, Falcao alisema ' mimi kucheza chini ya Mourinho?? hakuna kitu kama hicho na sina mpango huo kwasasa, kwasababu mimi na Mourinho ni vitu viwili tofauti kabisa'.
Kocha wa zamani wa Man utd, Sir Alex Ferguson ameingilia kati dirisha la usajili ili kumsajili mshambuliaji wa PSG Edison Cavani. Taarifa hizi zimeandikwa na Dailysport zikisema, Sir Alex aliongea na kocha wa PSG ambaye alishawahi kuwa kiungo wa kati ya Man utd, Laurent Blanc. Blanc alimwambia Sir Alex kuwa kwasasa klabu ya PSG haina mpango wa kumuuza mchezaji huyu, lakini watakuwa tayari kufanya hivyo mwishoni mwa msimu. Cavani aliyejiunga na PSG akitokea Napoli amekuwa akifichwa na Ibrahimovic kiasi ambacho kimefanya kiwango chake kisionekane. Taarifa zimesema kuwa tayari Moyes amekabidhiwa kiasi cha paundi mil 150 kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo na mwishoni mwa msimu ili kuimarisha kikosi chake.
Gazeti la Italia, Dello Sport, linasema Mkurugenzi Mtendaji wa Juventus, Beppe Marotta amekubali kumuuza mshambuliaji wa klabu hiyo Mirko Vucinic ndani ya dirisha dogo. Moratta ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na Dello sport na kusisitiza kuwa klabu yake haiwezi kumng'ang'ania mchezaji kama atataka kuondoka. Moratta amesema kama Arsenal na Vucinic watakubaliana yeye hata kuwa na kipingamizi chochote. Vucinic amekuwa dili kubwa kwenye dirisha dogo kutokana na upinzani anaoupata ndani ya klabu baada ya Tevez na Llorente kusajiliwa. Kusajiliwa kwa wachezaji hawa kumfanya Vucinic kukaa benchi muda mrefu jambo ambalo linamchukiza hivyo kutaka kuhama.
Kocha wa Everton, Roberto Martinez amesema beki wake wa kushoto Leighton Baines haondoki ndani ya klabu hiyo kwenye dirisha dogo wala mwisho wa msimu. Martinez amethibitisha hayo kwa msisitizo mkubwa na amesema mchezaji huyu anatarajiwa kusaini mkataba mpya wiki hii. Baines ni chaguo la Moyes kocha wa Man utd, na ameshapeleka maombi kwa Everton si zaidi ya mara tatu na yote yamekataliwa. Kama Baines atasaini mkataba mpya, basi ndoto za United kumsajili mwaka huu zitakuwa zimekufa. Baines anahitajika United ili aweze kuchukua namba ya Evra ambaye ameonekana kiwango chake kimeshuka.
No comments:
Post a Comment