Boniface Wambura, Ofisa Habari na Mawasiliano Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linawakumbusha makocha na maofisa habari wa klabu za Ligi Kuu kujiepusha na kauli za chuki, uchochezi na uongo kwa shirikisho na waamuzi kila timu zao zinapofanya vibaya kwenye mechi. Ni wajibu wa makocha kuzungumzia matokeo ya timu zao kiufundi badala ya kushambulia waamuzi na TFF kwa maneno makali. Pia maofisa habari nao wanatakiwa kuwa makini katika kauli zao kuhusiana na matokeo na masuala mengine. Kwa wale watakaokwenda kinyume TFF itawafikisha kwenye vyombo vya kinidhamu na maadili kwa ajili ya kuchukuliwa hatua stahiki.
No comments:
Post a Comment