Friday, January 24, 2014

Tetesi za usajili barani Ulaya 25 Jan 2014

Plane for all to see: Hulk, pictured with Zenit team-mate Luis Neto aboard a private jet, made a flying visit to England, posting this photo on Instagram from Luton Airport
Mshambuliaji wa Brazil na Zenit, Hulk akiwa pamoja na mchezaji mwenzake Luis Neto wakiwa ndani ya ndege wakielekea nchini England kushiriki moja kwa moja kwenye usajili wa dirisha dogo. Hulk hadi sasa anahusishwa na klabu za Chelsea na Man city, lakini hadi sasa haijajulikana anaelekea England kukutana na viongozi wa klabu ipi. Vyombo vingi vya habari vimesema Hulk huenda akawa anaelekea London kufanya mazungumzo na Chelsea, klabu ambayo imetajwa kumtoa Demba Ba na pesa juu kwa klabu ya Zenit ili kumsajili Hulk. 

Klabu ya Ac Milan imethibitisha kuwa kiungo mkabaji wa Chelsea, Michael Essien amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. Marca limeripoti kuwa klabu hizi mbili zitawajibika kumlipa mchezaji huyu nusu kwa nusu. Essien tokea arudi kwa mkopo akitokea Real Madrid hajaweza kupata muda wa kutosha uwanjani na nafasi hii ya kwenda Ac Milan itamuwezesha kupata mechi za kutosha zitakazompa uwezo zaidi wa kuitumikia nchi yake kwenye kombe la dunia. 

Klabu ya Liverpool imeanza kufanya mazungumzo na wakala wa winga wa Bayern Munich, Xherdan Shaqiri. Kumpoteza Mohamed Salah atakaye sajiliwa na klabu ya Chelsea wiki hii ndiyo sababu kubwa iliyoifanya klabu ya Liverpool kuhamia kwa Shaqiri ambaye kiuchezaji ni bora kuliko Salah. Changamoto za kumsajili mchezaji huyu ni kubwa kutokana na ukweli kwamba, kocha wa Bayern Munich, Pep Guardiola huwa anamtumia mara kwa mara kama mchezaji namba moja kwenye safu yake ya wachezaji wa akiba. 

Pichani (katikati) ni kocha msaidizi wa klabu ya Man utd,  Phil Neville akiwa na mashabiki wa klabu hiyo kwenye uwanja wa ndege kuelekea nchini Ujerumani kuangalia mechi kati ya Bayern Munich na Monchengladbach. Taarifa zinasema Neville atakutana na Moyes nchini Ujerumani na watakuwa wakimuangalia beki wa Munich, Dante. Mapema wiki hii Dante alikiri kuhusika kwenye mazungumzo na klabu ya Man utd. Ziara ya makocha hawa ni juhudi za kuweza kushinikiza uhamisho wake ili kuendelea kukiimarisha kikosi cha United baada ya Mata ambaye amesajiliwa wiki hii.

Raconteur? David Moyes (left) shares a joke with former Bayern manager Jupp Heynckes (centre)
Moyes akiwa nchini Ujerumani leo hii alipokutana na kocha wa zamani wa Bayern Munich Jupp Heynckes. Moyes na Neville wapo nchini Ujerumani kushinikiza usajili wa Dante. 

Incoming? Monchengladbach striker Max Kruse (left) is interesting United but Bayern's Dante (right) isn't
Dante

 Wilfried Zaha
DailyMail limethibitisha kuwa winga wa Man utd Wilfried Zaha amejiunga kwa mkopo na Cardiff City hadi mwisho wa msimu huu. Zaha anatarajiwa kufanyiwa vipimo na kuanza mazoezi wikiendi hii na Cardiff chini kocha mpya  Ole Gunnar Solskjaer. 

No comments:

Post a Comment