Klabu ya Arsenal imeshangazwa na kitendo cha benchi la ufundi la England kuendelea kumchezesha Wilshere akiwa majeruhi kwenye mechi ya kirafiki kati ya England na Denmark. Taarifa hii ya Arsenal imetolewa na madaktari wa timu baada ya kumfanyia vipimo mchezaji huyu na kugundua majeraha makubwa kwenye mguu wake wa kushoto baada ya kuchezewa rafu mbaya na beki wa Denmark, Daniel Agger. Wilshere alifanyiwa rafu dakika ya 12 ya mchezo lakini alitolewa nje dakika ya 59. Madakatri wa Arsenal wamesema benchi la ufundi la England lilitakiwa kuangalia uzito wa faulo aliyofanyiwa Wilshere na kumfanyia uchunguzi mdogo kabla ya kuamua kuendelea kumchezesha. Matokeo ya kuendelea kumchezesha yamesababisha kukua kwa majeraha na mchezaji huyu anatarajiwa kukosa mechi zilizobakia za ligi na anaweza pia kukosa kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment