Friday, March 29, 2013

Scholes, Jones na Nani wamerudi


Kocha wa Man utd amedhibitisha kupona kwa wachezaji wake watatu ambao ni Scholes, Jones na Nani. Sir Alex amesema wachezaji hao wamerudi kwenye kipindi kizuri ili kuipa timu nguvu ya kupambana na Chelsea kwenye FA na kuendelea kujiimarisha kileleni. Ferguson pia amefurahi kwani hakuna mchezaji wa Man utd hata mmoja aliyeumia kwenye international game zilizochezwa wiki hii. Sir Alex alisema “Kwasasa kikosi changu kipo full, nina wigo mpana wa kuchagua wachezaji watakaocheza”.  Man utd wikiendi hii itacheza na Sunderland siku ya jumamosi na jumatatu itakuwa darajani kucheza na Chelsea kwenye FA cup.

No comments:

Post a Comment