Mshambuliaji mwenye vituko nje na ndani ya uwanja Mario Balotelli, jana aliendeleza vituko baada ya kuonekana na taulo mbele ya waandishi wa habari mjini Geneva. Balotelli alifanya kituko hicho kwasababu anajua waandishi wa habari wakati wote wanamngojea kwa vituko. Ila wachezaji wenzake wa Ac Milan wamesema Balotelli amekuwa mtulivu toka ahamie Italy tofauti na alipokuwa England. Italy walikuwa Geneva wakicheza na Brazil katika mchezo uliokwisha kwa sare ya goli mbili, katika mchezo huo Balotelli alifunga goli moja.
hahahahaha
ReplyDelete