Friday, March 29, 2013

Tanzania yafagiliwa na FIFA


FIFA imeanza kuitambua vyema Tanzania baada ya kichapo ilichotoa kwa Morocco, hali hiyo imejionesha baada ya FIFA kuirusha hewani Tanzania kupitia official website yake kama inavyooneka kwenye picha. FIFA imesema kiwango cha soka la Tanzania kimependa sana kutokana na mipango yake mizuri ya kuanza kuwekeza kwenye timu za vijana chini ya miaka 15 na 17. Zaidi, FIFA imemtaja kocha Poulsen kuwa ni moja ya chachu ya maendeleo ya soka Tanzania baada ya kuijenga vyema timu Taifa Stars na timu ya vijana chini ya miaka 20. Wikendi iliyopita Taifa Stars iliifunga Morocco goli tatu kwa moja kwenye mchezo wa kuwania kufuzu kombe la dunia,matokeo ambayo FIFA imesema yataipandisha Tanzania kwenye renki za viwango ya FIFA mwezi ujao. Tanzania oyeeeee!!!!!!

No comments:

Post a Comment