Klabu ya Azam FC leo imesafiri kwenda nchini Morocco kucheza na AS FAR katika mchezo wa marudiano kwenye michuano ya washindi barani Afrika. Katika mchezo wa kwanza uliofanyika jijini Dar es salaam, Azam FC na AS FAR zilitoka droo ya bila kufungana hivyo basi Azam FC inatakiwa kutoka droo yoyote ya magoli au kushinda katika mchezo wake wa marudiano jijini Rabat. Azam FC wameondoka leo na ndege ya shirika la Emirate wakipitia Dubai ikiwa wachezaji wawili wamebaki akiwemo Nuhu Eliye ambaye ni majeruhi pamoja na Ibrahim Shikanda anayeelekea jijini Nairobi nchini Kenya kwenye masomo.
No comments:
Post a Comment