Tuesday, April 16, 2013

Mechi ya Simba vs Azam yaingiza mil 66 - TFF

Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Azam na Simba iliyochezwa Aprili 14 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 66,855,000 kutokana na watazamaji 11,458. Viingilio katika mechi hiyo namba 155 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 15,587,177.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 10,198,220.34. Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 7,925,683.45, tiketi sh. 3,818,890, gharama za mechi sh. 4,755,410.07, Kamati ya Ligi sh. 4,755,410.07, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,377,705.03 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,849,326.14. 

No comments:

Post a Comment