Tuesday, April 9, 2013

Azam yawakaribisha Nyoni na wenzake

Club ya Azam FC imetangaza kuwakaribisha kundini wachezaji wake wanne Munishi, Nyoni, Morad na Morris baada ya kuwa kwenye tuhuma ya kupokea rushwa ya shilingi milioni saba kutoka kwa viongozi wa Simba ili wapange matokeo katika mchezo baina ya timu hizo uliofanyika tarehe 27 Oktoba mwaka jana 2012. Azam fc kupitia kocha wake Stewart Hall wamewakaribisha kwa furaha wachezaji hao baada ya kusimamishwa kwa muda mrefu. Azam imewaruhusu wachezaji hao kurudi kikosini baada ya TAKUKURU kutoa taarifa kuwa haijadhibitisha tuhuma za rushwa dhidi ya wachezaji hao. Kurudi kwa wachezaji hawa ambao ni muhimu kwa klabu hiyo, wataiwezesha Azam kupambana vyema katika kugombania ubingwa wa ligi kuu Vodacom Tanzania bara.  

No comments:

Post a Comment