Saturday, August 3, 2013

Arsenal isipoangalia Madrid watamuiba Suarez

You should stay: Ian Wright has told Luis Suarez to stay in Liverpool rather than move to Arsenal
Star Sport linaripoti kuwa klabu ya Arsenal inatakiwa kukamilisha mapema usajili wa Luis Suarez ili kuipiku Real Madrid ambayo ina mpango wa kumsajili mchezaji huyu baada ya kukamilisha usajili wa Bale. Star Sport linasema, baada ya Madrid kukamilisha safu yake ya benchi la ufundi kwa kumchagua Ancelotti na Zidane kuwa makocha, hatua inayofuata ni kumsajili Gareth Bale wa Tottenham, kwani ndiye chaguo lao la kwanza, na mara Bale atakapotua BernabĂ©u, mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ndiye atakayefuata. 'Madrid ni klabu tajiri, paundi mil 50 za Suarez sio kitu, hivyo Arsenal kama wanamhitaji Suarez wakamilishe usajili mapema', Star Sport limeripoti taarifa hii ili kuishauri klabu ya Arsenal ambayo bado inasuasua kumsajili Suarez. 

Klabu ya Arsenal hadi sasa imeshazidiwa kete na klabu pinzani kwa zaidi ya wachezaji wawili. Sababu kubwa ya kuzidiwa kete ni kushindwa kukubaliana kwenye masuala ya kifedha. Moja ya wachezaji ambao Arsenal ilizidiwa kete ni Jovetic ambaye amesajiliwa na Man city baada ya Arsenal kushindwa kukubaliana na Fiorentina,  pia Gonzalo Higuian aliyesajiliwa na Napoli baada ya Arsenal kushindwa kukubaliana na Madrid. Hali hii inaweza pia kujitokeza kwa Suarez, kwani hadi sasa usajili wa mchezaji huyu kwenda Arsenal unashindikana kwasababu Arsenal wametoa ofa ya paundi mil 40, wakati klabu ya Liverpool inahitaji paundi mil 50. 

No comments:

Post a Comment