Friday, June 28, 2013

Lazima tumsajili Gareth Bale - Raisi wa Madrid

Raisi wa Real Madrid, Florentino Perez amewahakikishia mashabiki wa klabu hiyo kuwa mchezaji wa Tottenham Gareth Bale lazima atue Bernabeu. Akiongea na gazeti la AS, Perez alisema ‘Gareth Bale ni lazima tumsajili kwasababu benchi la ufundi pamoja na mashabiki wanamtaka, na mimi kama raisi natakiwa kutekeleza mahitaji yao kwani nipo hapa kwa ajili yao. Bale ni mchezaji mzuri, na akiungana na Ronaldo timu yetu itakuwa madhubuti na yenye ushindani mkubwa. Tumeshaanza mazungumzo na Tottenham naamini tutafikia muafaka mapema’. Kwa mujibu wa Zinedine Zidane ambaye ni kocha msaidi wa Madrid, ni kwamba klabu hiyo imeshatuma maombi kwa Tottenham ili kumsajili Bale kwa ada ya Euro mil 60, lakini hadi sasa klabu Tottenham haijawajibu Madrid. Taarifa kutoka kwa mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy imesema hadi sasa hawajatoa jibu kwa Madrid kwasababu Bale sio mchezaji wa kuuzwa na hata kama wakimuuza ni zaidi ya Euro mil 100.  

No comments:

Post a Comment