Saturday, April 6, 2013

Bayern Mabingwa Bundes

Club ya Bayern Munich leo imetwaa ubingwa wa ligi kuu ya Germany baada ya kushinda  mechi yao dhidi ya Eintracht Frankfurt kwa goli moja kwa bila. Ushindi huu unaifanya Bayern ifikishe vikombe 23 vya ligi, vilevile Bayern leo wameweka historia katika soka la Ujerumani baada ya kutangazwa mabigwa wakiwa na mechi sita mkononi. Baada ya kutwaa kombe la ligi, Bayern Munich kwasasa wataelekeza nguvu zao zote kwenye club bingwa (UEFA Champions) wakiwa wamebakiza mchezo wa marudiano dhidi ya Juventus baada ya kushinda mechi yao ya nyumbani kwa goli 2 kwa bila. Katika mechi hiyo Bayern wanapewa nafasi kubwa ya kusonga mbele licha ya upinzani mkali itakayoupata kwa Juventus. Bayern Munich ilifika fainali ya UEFA msimu uliopita lakini walitolewa kwa mikwaju ya penati na Chelsea. Mbali ya kufika fainali msimu uliopita Bayern Munich imendelea kuonesha mchezo mzuri msimu huu na ni moja ya timu ambazo zinafikiriwa kushinda kombe la ulaya tofauti na historia inavyoonesha kuwa timu nyingi zinazofika fainali UEFA msimu unaofuata zinaishia robo fainali au kwenye makundi
Wachezaji wa Bayern wakishangilia ubingwa

No comments:

Post a Comment