Sunday, April 7, 2013

Eric Abidal amerudi, baada ya kufanyiwa upasuaji

Abidal akisali kabla ya kuingia
Eric Abidal (33) beki wa Barcelona jana alicheza mechi yake ya kwanza baada ya kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwaka mmoja tokea Machi mwaka jana (2012). Abidal alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ambapo alifanyiwa upasuaji na kufanikiwa kubadilishwa ini. Baada ya upasuaji Abidal alijumuika na familia yake kwa kipindi kirefu kabla ya kujiunga tena na club yake ambapo alianza kufanya mazoezi madogo madogo ikiwemo kucheza kwenye mechi za kirafiki za timu ndogo ya Barcelona B. Akirudi katika timu ya kwanza Abidal aliingia dakika ya 69 kipindi cha pili (mechi kati ya Barcelona 5 - 0 Mallorca) ambapo Gerard Pique alitoka na Abidal kuingia, uwanja mzima ulisimama kumpokea Abidal kwa kupiga makofi lakini kabla ya kuingia Abidal aliinamisha shingo akiwa amejishika kifuani kumshukuru Mungu. Abidal alipokuwa akihojiwa baada ya mechi alisema “nimefarijika sana kwa mapokezi Nou Camp, vilevile nawashukuru sana wazazi wangu, mke wangu, marafiki na mashabiki wote wa Barcelona kwa msaada wao, kwani bila wao nisingeweza kurudi tena uwanjani”. Kurudi kwa Abidal ni furaha kwa Vilanova kocha mkuu wa Barca kwani timu yake inaudhaifu mkubwa kwenye safu ya ulinzi, uwepo wake utaisaidia sana Barca hasa kwenye mashindano ya UEFA ambapo wiki ijayo Barcelona watakuwa nyumbani kuwakaribisha PSG baada ya kutoka droo ya goli 2-2 katika mchezo wa kwanza jijini Paris. 

No comments:

Post a Comment