Thursday, April 4, 2013

Hali ya Uwanja wa Bukoba

Kwenye picha ni uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, ni uwanja unaotumika kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara. Uwanja huu una uwezo wa kuchukua watu 8000, kuta zake ni fupi na hakuna uzio wa kutenganisha sehemu ya kuchezea na watu wanapokaa. Mazingira haya ni ya hatari kiusalama kwa wachezaji na waamuzi. Kiwanja kimezungushiwa uzio mfupi, mtu aliye nje ni rahisi kuangalia mpira bure. Club ya Kagera Sugar ndiyo inatumia uwanja huu kama uwanja wa nyumbani, club hii itajiendesha vipi kama asilimia kubwa ya watazamaji wanaangalia bure na wale wanaoingia ndani ni watu 8000 tu. Hii ni tafakari tu ya mazingira halisi ya soka la bongo. Picha za chini zinaonesha uwanja huo ulivyo. 

No comments:

Post a Comment