Mshambuliaji tegemezi wa Barcelona Lionel Messi anategemewa
kucheza kwenye mechi ya nusu fainali ya kwanza kati ya Bayern Munich na Barcelona
inayotarajiwa kufanyika wiki ijayo jijini Munich. Messi aliyepata maumivu ya
misuli kwenye mguu wake wa kulia katika mechi ya kwanza kati ya PSG na Barcelona
amekuwa kwenye matibabu kwa kipindi cha wiki tatu sasa licha kucheza kipindi
cha pili katika mechi ya marudiano dhidi ya PSG. Messi alipewa taarifa za
kupona kwake kutoka kwa daktari wa klabu akiwa kwenye mazoezi jumanne ya wiki
hii. Messi ameshakosa mechi mbili za ligi na anatarajiwa kutokucheza mechi
yoyote akingojea mechi dhidi ya Bayern Munich ili kuepusha majeraha ya aina
yoyote kwa mchezaji huyo ambaye ni chachu kwa Barcelona kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment