Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Liverpool Ian Ayre
amesisitiza kuwa Luis Suarez hatouzwa mwishoni mwa msimu huu. Ayre aliyasema hayo
alipohojiwa kuhusu tetesi zilizopo kuwa Suarez atauzwa kwenda Bayern Munich,
PSG au Man City, Ayre alisema “ili Liverpool iweze kushinda kombe la ligi na
kushiriki michuano ya ulaya lazima iwe na wachezaji kama Suarez na Gerrard, hivyo Liverpool haiwezi kumuuza Suarez, kwasasa tupo kwenye kipindi
cha kuimarisha timu yetu, tumefanya usajili mzuri mwezi January, timu yetu
imeimarika zaidi na tutaendelea kufanya usajili lakini sio kuuza wachezaji
mahili kama Suarez. Suarez amehusishwa sana kuihama Liverpool katikati ya msimu
huu baada ya Liverpool kufanya vibaya kwenye ligi kuu kitu ambacho
kimeelezwa kuwa Suarez hajakifurahia hivyo atapenda kujiunga na klabu kubwa ili
akuze zaidi kipaji chake na kushinda vikombe.
No comments:
Post a Comment