Friday, April 5, 2013

Sina mpango wa kuihujumu Simba - Nyange

Geofrey Nyange makamu mwenyekiti wa Simba aliyejiuzulu amesema hawezi kuihujumu club ya Simba katika mechi zake zilizobakia. Nyange amesema hayo alipokuwa akihojiwa na Mwananchi ambapo amesisitiza kuwa yeye hana mpango wa kuihujumu timu ya Simba kwani kitendo hicho kitamfanya achukiwe na wapenzi wa Simba. Nyange alisema hayo ni maneno ya watu wachache wanaotaka kumgombanisha yeye na wanachama wa Simba kitu ambacho sio kizuri. Nyange alimalizia kwa kusema tatizo lililopo Simba ni mapengo ya wachezaji, "kuna wachezaji wameondoka Simba hadi leo nafasi zao hazijazibwa ndiyo maana timu haifanyi vizuri, Okwi, Mafisango na Yondani wote hawapo nafasi zao kaziba nani" alihoji Nyange, amesisitiza kuwa mapengo hayo ndiyo chanzo cha Simba kupata matokeo mabaya. Nyange alisema yeye bado ni mwanachama halali wa Simba na yupo tayari wakati wowote kuingoza Simba lakini mpaka matatizo yaliyopo yatatuliwe. 

No comments:

Post a Comment