Sunday, April 7, 2013

Uchambuzi, Kucheza soka vs Uvutaji sigara baada ya Balotelli kupigwa faini


Mshambuliaji wa Ac Milan Mario Balotelli wikiendi hii ameshikwa na wasimamizi wa treni akiwa kwenye choo cha treni anavuta sigara. Kampuni ya treni imesema itampiga faini kwa kitendo alichokifanya kwani uvutaji wa sigara ni marufuku kwenye treni za Italia. Ac Milan walikuwa safarini kwenda kucheza na FIorentina katika mechi iliyoisha kwa droo ya goli mbili kwa mbili.
Tukiliangalia kwa undani swala la uvutaji wa sigara kwa mchezaji wa mpira linaonesha dhahiri kuwa Mario Balotelli anaelekea kuharibu kipaji chake kwasababu uvutaji wa sigara unaleta madhara makubwa kwenye mapafu ambavyo ni viungo muhimu kwa mwanadamu kumwezesha kuhema/kupumua. Ikumbukwe kuwa mchezaji yoyote wa michezo ya kutumia nguvu kama soka anahitaji mapafu yenye afya njema ili kumpatia uwezo wa kustahimili harakati za mpambano ndani ya kiwanja. Lakini kwa upande wa Balotelli itamchukua muda mfupi kuchoka kucheza soka kwani sigara ina tabia ya kula kwa kasi mapafu na hata kusababisha kansa ya mapafu kitu ambacho ni hatarishi kwa ajira yake. 
Balotelli akiwa na sigara mkononi
Wachezaji wengi ndani na nje ya nchiwamepoteza sifa zao na hatimaye kuachana na soka kabisa kwasababu ya uvutaji wa sigara wakiwemo Johan Cruyff, Jack Charlton na Jackie Milburn. Johan Cruyff alifikia hatua ya kuvuta sigara 20 kwa siku, kitendo ambacho kilimfanya aachane na soka akiwa na rekodi nzuri ya kuwa mchezaji bora wa FIFA mara tatu, hii leo Cruyff ni balozi wa kupambana na uvutaji wa sigara kwa wachezaji. Clubs zote ulaya zinakataza wachezaji kuvuta sigara kwani wanajua kitendo hicho kitawafanya waishiwe mapema, lakini imekuwa vigumu sana kusimamia sheria hiyo ikiwa sio rahisi kumfuatilia mchezaji mmoja mmoja hadi anavyoishi nyumbani kwake. Kwasasa wachezaji ambao wameshashikwa mara kadhaa wakivuta sigara ni pamoja na Rooney, Berbatov, Macheda, Balotelli, Buffon, Nesta na Laquinta. Wachezaji wote hawa uwezo wao umeshuka sana sababu mojawapo ikiwa ni uvutaji wa sigara kupita kiasi. 

No comments:

Post a Comment