Sunday, April 7, 2013

Man utd vs Man city, upinzani ni upinzani tu

Leo tarehe 8 mwezi April, ni siku iliyongojewa kwa hamu kubwa ili kumaliza ubishi wa nani mbabe kati ya Man utd na Man city kwa msimu huu. Washabiki wengi wa Man city wamekuwa wakisema Man utd wamebahatisha tu msimu huu ila kiwango hawana, leo itakuwa ni siku ya wao kudhibitisha hilo wakiwa ugenini kucheza mchezo wao wa 31.
Man utd wakiwa na pointi 77 nafasi ya kwanza wakati wapinzani wao Man city wana point 62 nafasi ya pili tofauti ya pointi 15. Kwa kawaida mchezo kama huu unakuwa hauna msisimko mkubwa ikiwa Man utd wako mbele kwa pointi nyingi ambazo sio rahisi kufikiwa lakini mchezo huu unakutanisha mahasimu wakubwa England Man utd na Man city zikiwa ni timu zinazotoka mji mmoja wa Manchester hivyo mchezo utakuwa wa ushandi mkubwa kila timu ikitafuta kulinda heshima yake. Katika mchezo wa raundi ya kwanza Man utd walishinda kwa goli 3-2. 

Sir Alex alipohojiwa kuhusiana na mechi ya leo, alisema “najua haitakuwa mechi ya kubeza, Man city wanakuja kwa nia ya kutuabisha, lakini sisi tumejipanga”. Roberto Mancini yeye alisema “hii mechi sio ya muhimu kwa kushindania kombe la ligi, lakini mjue upinzani ni upinzani wakati wote, tunataka kuwaonesha hatukustahili kuwa nyuma kwa pointi 15, tunaweza kuzipunguza licha ya kuwa najua Man utd ni mabingwa tayari”, naye Joe Hart (Man city) alisema ubingwa tumeukosa ila tunataka kuwafurahisha mashabiki wetu” . Mchezo wa leo unatarajiwa kufanyika saa nne usiku kwa masaa ya Afrika mashariki na kati.    

No comments:

Post a Comment