Waziri wa Habari Utamaduni na
Michezo Dk. Fenella Mukangara ameunda kamati ya wajumbe kumi na moja (11)
itakayokuwa na kazi ya kuhakikisha timu ya Taifa (Taifa Stars) inashinda. Taifa
Stars iliyopo kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kucheza kombe la dunia nchini
Brazil mwaka 2014 inahitaji kuendeleza ushindi ili iweze kufuzu. Katika
kuhakikisha inapata ushindi waziri wa michezo ameamua kuunda kikosi
kazi kinachojumusha wajumbe kumi na moja ambao Mohamed Dewji (Mb), Mkuu wa ZSSF
Dk Ramadhani Dau, Rais wa TFF Leodegar Tenga, Mwenyekiti wa BMT Dioniz Malinzi,
Zitto Kabwe (Mb), George Kavishe, Mohamed Raza (Mb), John Komba (Mb), Teddy
Mapunda, Abji Shabir na Joseph Kusaga. Hakika hii ni timu kazi kwani imehusisha
wajumbe wengi ambao ni wapenda soka na wenye fursa mbalimbali zinazoweza
kuisaidia Stars kushinda katika mechi zake zilibakia.
No comments:
Post a Comment