Saturday, April 27, 2013

Yanga inashikilia rekodi ya ubingwa Tanzania bara

Klabu ya Yanga imefanikiwa kutwaa ubingwa wa 24 mwaka huu, ubingwa ambao tangu kuanzishwa kwa Ligi Kuu Tanzania bara hakuna timu yoyote Tanzania bara inayokaribia ikiwa nafasi ya pili inashikiliwa na watani wa jadi Simba SC kwa kuwa wametwaa ubingwa huo mara 18 tu. Rekodi ya Ubingwa wa Yanga :1968, 1969, 1970, 1971, 1972, 1974, 1981, 1983, 1985, 1987, 1989, 1991, 1992,1993, 1996, 1997, 1998, 2002, 2005, 2006, 2007-2008, 2008-2009, 2010-2011, 2012-2013. Hii inamaanisha Simba bado wanakazi kubwa ya kuweza kuwafikiwa wapinzani wao kwani watahitajika kushinda mara sita ili kuwafikia Yanga. 

Pamoja na kutangazwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013, kikosi cha timu ya Young Africans leo kimeendelea na mazoezi ya viungo na kujenga misuli (GYM) katika kituo cha mazoezi kilichopo jengo la Quality Cetntre kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union siku ya jumatano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Uongozi wa klabu ya Yanga unawaomba wanachama, wapenzi na washabiki wa timu ya Yanga kujitokeza kwa wingi siku ya jumatano (mei mosi) katika dimba la uwanja wa Taifa ili kuja kuwashangilia vijana wakiendeleza furaha ya kutwaa Ubingwa wa VPL msimu huu.

No comments:

Post a Comment