Kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah yupo kwenye
wakati mgumu kuwashawishi Kevin Prince Boateng na Michael Essien warudi kwenye
kikosi cha timu ya Taifa ili kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Ghana
kinachopigania nafasi moja kati ya tano kutoka nchi za Afrika kwenye michuano
ya kombe la dunia mwakani nchini Brazil. Boateng na Essien waliojitoa kwenye
timu ya taifa kwa madai ya sababu za kiafya mwaka 2011, kwasasa wanaonekana kuwa
“fiti” kiafya lakini hawajawa tayari kuichezea Ghana. Kocha wa Ghana Appiah
amesema yupo tayari kuwabembeleza wachezaji hao hadi dakika za mwisho kwani ni
wachezaji anaowahitaji kipindi hiki ili kuimarisha timu yake. Appiah alisema “
Essien na Boateng ni wachezaji wazuri, ila kwasasa hawapo tayari kucheza timu ya
taifa, lakini mimi nitawafuata huko walipo kuongea nao ili warudi, naamini
nitafanikiwa na timu yangu itaimarika’. Lakini uchambuzi unaonesha nchi za Ulaya na
Amerika wachezaji wao wanajisikia fahari kucheza kwenye timu za taifa kitu ambacho ni
tofauti kwa wachezaji wa Afrika, hii ni kutokana na matunzo mabaya kwa
wachezaji wa timu za taifa Afrika lakini pia wachezaji wa Afrika hawana utaifa
kwa mataifa yao.
No comments:
Post a Comment