Monday, May 20, 2013

Angalia video ya Alex Song alivyotia aibu

Angalia video inayomuonesha Alex Song alivyoingiwa na aibu baada ya kudhania anapewa yeye kombe na Puyol baadala ya Abidal. Tukio hilo lilitokea usiku wa jumapili siku ambayo Barcelona walikabidhiwa kombe la ubingwa wa ligi. Nahodha wa klabu hiyo Puyol ndiye alikabidhiwa kombe na uongozi wa la liga lakini hakulinyanyua na kuamua kumpatia Abidal na kocha Vilanova kombe hilo baada ya wawili hao kupata nafuu ya kansa lakini Puyol alipokuwa anaelekea kumpatia Abidal kombe Alex Song alidhania anapewa yeye akajitokeza kwa mbele jambo ambalo lilimfanya Puyol amvute mkono Abidal na kumuacha Song anacheka kwa aibu. Angalia video...



No comments:

Post a Comment