Tuesday, May 21, 2013

Kocha wa Stoke City ajiuzulu

Long stint: Pulis guided Stoke to the Premier League for the first time in 2008
Tony Pulis kocha mkuu wa Stoke City ametangaza kuacha kazi ya kuifundisha klabu hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka saba. Pulis ametangaza uamuzi huo baada ya kukutana na mmliki wa klabu hiyo Peter Coates na kukubaliana. Hata hivyo imeelezwa kuwa Pulis alishawaambia viongozi wa Stoke kuwa mwishoni mwa msimu huu ataacha kazi lakini hakuwa tayari kutangaza hadharani uamuzi wake hadi ligi itakapomalizika. Hadi sasa haijajulikana sababu zilizomfanya Pulis ajiuzulu na hajasema anatarajia kwenda klabu gani baada ya hapo licha ya kuwa wiki iliyopita Pulis alionekana nchini Hispania akiangalia mechi kati ya Real Sociedad na Granada.

No comments:

Post a Comment