Friday, June 28, 2013

Maandamano ya jana usiku nchini Brazil kiboko

Maandamano ya wanaopinga kufanyika kwa michuano ya kombe la dunia na kombe la mabara nchini Brazil, yaliendelea tena jana usiku kwa kufanya maandamano makubwa zaidi hadi kufikia sehemu za viwanja ambavyo vinatumika kwenye michuano ya kombe la mabara inayoendelea hivi sasa nchini Brazil. Waandamanaji hao wanapinga serikali ya Brazil kutumia fedha nyingi kwenye michuoano hii wakati huduma za kijamii ni duni. Jumapili ijayo itakuwa ni fainali ya michuano hii wakati Brazil watakutana na Hispania, mchezo ambao utafunikwa na maandamano makubwa zaidi nia ikiwa ni kusimamisha mchezo huo usifanyike. Lakini serikali ya Brazil imesema itahakikisha inawazuia waandamanaji hao kufika sehemu yoyote ambayo itaathiri mchezo huo. Zifuatazo ni picha mbalimbali za maandamano ya jana usiku. 

The future's orange: Protesters set cars and stores on fire during a demonstration near the stadium in Belo Horizonte
Demonstration: Police use tear gas against protestors in Brasilia but that is hardly FIFA's fault
Poverty and deprivation: But FIFA were right to award Brazil the World Cup

No comments:

Post a Comment