Winga wa PSG David Beckham ametangaza rasmi kustaafu soka
mwishoni mwa msimu huu. Beckham mwenye umri wa miaka 38 ametangaza uamuzi huo
leo akiwa ameshacheza zaidi ya mechi 100 na timu ya taifa, vikombe sita vya
ligi kuu ya Uingereza akiwa na Man utd na vikombe vingine vitatu vya ligi ya Hispania,
Marekani na Ufaransa akiwa na timu za Madrid, Galaxy na PSG. Beckham alianza
kucheza soka akiwa na miaka 14 alipojiunga na Man utd mwaka 1993 hadi
mwaka 2003 alipohamia Real Madrid na mwaka 2007 alihamia Galaxy nchini
Marekani. Mwaka 2009 hadi 2010 alikwenda Ac Milan kucheza kwa mkopo na mwaka 2013 alihamia PSG ambapo ameshacheza
mechi tisa hadi sasa. Beckham hadi sasa ni mchezaji pekee barani Ulaya ambaye
ameweza kushinda kombe la ligi na timu nne tofauti na pia ni mchezaji ambaye
ameshacheza kwenye ligi tatu kubwa barani ulaya (ligi ya Uingereza, Hispania na
Ufaransa). Katika maneno yake na
waandishi wa habari Beckham amesema “nashukuru nimeweza kucheza hadi muda huu,
imefikia kipindi sasa niwaachie wengine kwasababu siwezi tena kucheza kwenye
kiwango changu cha juu, nawashukuru PSG kwa kunisajili kwenye kipindi hiki
lakini imefikia muda nipumzike kwenye soka ili niweze kufanya shughuli zingine”.
Mbali na soka Beckham pia anafanya shughuli nyingi ikiwemo mitindo na kufanya
matangazo mbalimbali ya bidhaa na huduma za makampuni. David Beckham na mkewe
Victoria hadi sasa wana watoto wanne Brooklyn Joseph (alizaliwa 1999 London),
Romeo James (alizaliwa 2002 London),
Cruz David (alizaliwa 2005 Madrid); na binti yao mmoja Harper Seven (alizaliwa 2011,Los
Angeles)
No comments:
Post a Comment