Thursday, May 16, 2013

Vijembe vya mechi ya Simba na Yanga

Klabu ya Simba imeendelea kupondwa na washabiki mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wa Yanga na wa timu zingine za ligi kufuatia mchezo wa jumamosi wakisema Simba haina uwezo wa kuifunga Yanga. Hii imekuja kufuatia uamuzi walioufanya klabu ya Simba kuamua kuwapa vijana nafasi ya kuonesha uwezo wao kwani kikosi cha Simba kinachotarajiwa kushuka dimbani siku ya jumamosi kitajaa wachezaji wadogo ambao wamesekana hawana uzoefu zaidi ya wachezaji wa Yanga. Maneno hayo yalianzia kwa wazee wa Yanga ambao walitoa kauli yao mbele ya waandishi wa habari wakisema “Mnyama ajiande kuuwawa jumamosi” lakini vilevile kocha mkuu wa Azam kupitia Mwananchi alisema "Simba inategemea nguvu ya mashabiki kushinda lakini sio uwezo wa wachezaji" na kauli zinazolingana na hizi zimetolea vilevile na baadhi ya mashabiki wa Yanga. Kufuatia kauli hizi viongozi mbalimbali wa Simba akiwemo mwenyekiti Aden Rage amewahakikishia wapenzi wa Simba wasiwe na wasiwasi kwani vijana wapo tayari kuiangamiza Yanga na kusisitiza wajitokeze kwa wingi siku ya jumamosi. Mbali na kauli hii ya rage na viongozi wengine wa Simba lakini bado wadau wengi wa soka nchini hawajiridhishi ndani ya fikra zao kuwa Simba itaweza kushinda mchezo dhidi ya Yanga kwa kutumia vijana wadogo licha yakuwa wanaamini inaweza kutokea muujiza Yanga wakafungwa, hivyo mchezo huo wa jumamosi kati ya Simba na Yanga unangojewa na wengi ili kutegua maswali yanayowazunguka wadau wa soka nchini. 

No comments:

Post a Comment