Thursday, May 23, 2013

Eboue na Toure kuikosa Taifa Stars

Mabeki Emmanuel Eboue na Kolo Toure wamefungiwa kucheza mechi za timu ya taifa ya Ivory Coast zilizobakia kwa kosa la utovu wa nidhamu. Wachezaji hao wamefungiwa kucheza dhidi ya Taifa stars na Gambia kwenye michuano wa kuwania kushiriki kombe la dunia kwenye mechi ambazo zinazotarajiwa kufanyika mwezi ujao (Juni). Eboue na Kolo wamefikwa na adhabu hiyo baada ya kukiponda chama cha soka cha Ivory Coast na kumkejeli kocha wa taifa Sabri Lamouchi kwenye vyombo vya habari wakijikweza kuwa wao nitegemeo kwenye safu ya ulinzi wa timu hiyo na hawakustahili kukosa kwenye mechi yao ya awali dhidi ya Gambia. Kufuati utovu huu wa nidhamu shirikisho la soka nchini Ivory coast lilimwambia kocha Lamouchi kuwasimamisha wachezaji hao hadi waombe msamaha. 

No comments:

Post a Comment