Thursday, January 16, 2014

Tetesi za usajili Ulaya leo 17 Jan 2014

Kinda wa Chelsea, Kevin De Bruyne yupo nchini Ujerumani kufanyiwa vipimo na klabu ya Wolfsburg kabla ya kusaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo 

 
Baada ya Benfica kutoa ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Madrid, Morata, klabu ya Inter Milan pia imetuma ofa ya Euro mil 13 ili kumnasa mchezaji huyu. Kabla ya klabu hizi kutuma ofa zao, klabu ya Arsenal ndiyo ilikuwa ya kwanza kutangaza nia ya kutaka kumsajili. Lakini chelewa chelewa ya Arsenal inaweza kusababisha kumkosa Morata ambaye klabu nyingi zimeonesha nia ya kutaka kumsajili. 

 
Mbali nia ya kutaka kumsajili Pogba na Vidal kutoka klabu ya Juventus, klabu ya Man utd pia imeripotiwa kutaka kumsajili kiungo wa Napoli Marek Hamsik akiwa kama mbadala kama dili la Pogba na Vidal litagonga mwamba. 

Taarifa za kinda wa Man utd Fabio kujiunga na Cardiff kwa mkopo zimeshaanza kuthibitishwa na baadhi ya vyombo vya habari na imesemekana muda wowote dili hili litatangazwa rasmi. 

Clarence Seedorf ameshawasili nchini Italia akitokea Brazil tayari kuchukua mikoba ya Massimiliano Allegri ili kuifundisha klabu ya Ac Milan akiwa kama kocha mkuu baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka kumi, 

Gazeti la michezo la nchini Ujerumani Bild linaripoti kuwa klabu za Man utd na Real Madrid zimetuma ofa ya kutaka kumsajili kiungo wa Dortmund, Ilkay Gundogan. Haikutajwa ni kiasi gani klabu zote zimetuma, lakini taarifa zinasema kiungo huyu anaweza kuondoka ndani ya dirisha dogo kwenda Man utd au Madrid. Juhudi za klabu husika ndiyo zitafanikisha uhamisho wa Gundogan, kwani mchezaji mwenye amekiri kupokea maombi kutoka kwa klabu zote na amesema yeye hana tatizo lolote kuhamia Man utd au Madrid, bali ni makubalino kati yao na klabu yake ndiyo jambo la muhimu.  

Nani Anderson
Wachezaji watatu wa Man utd Anderson, Vidic na Nani bado wameendelea kutajwa na vyombo vya habari kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho na klabu mbalimbali ili wahame United. Anderson yupo kwenye mazungumzo na klabu za Fiorentina na Juventus wakati Nani yupo kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho na klabu ya Sporting Lisbon. Nemanja Vidic mazungumzo yake bado yapo kwenye hatua za awali kutokana na ofa nyingi alizopata kutoka klabu mbalimbali. Klabu ambazo zinamhitaji Vidic hadi sasa ni Barcelona, Juventus, PSG, As Roma na Monaco. Lakini kati ya hawa wachezaji watatu, Anderson na Nani ndiyo wapo kwenye nafasi kubwa ya kuhama kuliko Vidic.  

No comments:

Post a Comment